Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 15, 2014

Mtu mmoja anayesadikaki ni jambazi wa kutumia silaha ameuwawa kikatili na wananchi wenye hasira

KILIMANJARO Katika tukio la kusikitisha ambapo mtu mmoja aliyejulika kwa jina la Wence Martine (38) ameuwawa kikatili kwa kukatwakatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi wenye hasira kali waliomtuhumu kuwa ni jambazi wa kutumia silaha.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Moita Koka, Alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 14 majira ya saa 05:30 mwaka 2014, katika eneo la Majengo tarafa ya Moshi Mshariki Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo wananchi hao walijichukua sheria mkononi kwa kumkatakata kijana huyo na mapanga hadi kumsababishia kifo.

Aliongeza kusema kuwa upelelzi unaendelea na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi, kwa ajaili ya kusubiri taratibu za mazishi.

No comments:

Post a Comment