Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 15, 2014

Halmashauri ya manispaa ya Moshi imetakiwa kutoa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi

KILIMANJARO halmashauri ya manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro imetakiwa kutoa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi hatua ambayo itawawezesha kulipa kodi kwa wakati hususani za majengo na kuondokana na usumbufu ambao hupelekea kutaifisha mali za wananchi.

Hayo yalibainishwa na Diwani wa kata ya Mji mpya Abuu Shayo, wakati wa mkutano  wa adhara wa wananchi na  serikali za mitaa uliofanyika jana katika uwanja wa mtaa wa Kwakomba mjini Moshi.

Shayo alisema ni vema halmashauri ya Manispaa ya Moshi kupitia watendaji wake kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi za majengo na kuacha tabia ya kutaifisha mali za wananchi hao pasipo utoaji wa elimu.

Alisema wananchi wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kutokana na baadhi ya viongozi wa halamshauri kutokuwa na desturi ya kuwakumbusha wananchi jambo ambalo limekuwa likiibua migogoro kati ya serikali na wananchi wakati wa ukusanyaji wa kodi hizo.

Aidha diwani Shayo aliwataka wenyeviti wa mitaa na watendaji wa kata kutoa elimu hiyo kupitia mikutano mbalimbali ili kuepusha migogoro isiyo yalazima kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Mtendaji wa kata hiyo Leonis Bura, alisema zaidi ya shilingi milioni 150 zinahitajika katika ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya Mjipya  kwaajili ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi.

 Kwa Upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Kwakomba Matias Mosha, aliwataka wananchi kuwa na desturi ya kuchangia miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kuitegemea serikali kwani maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe.


No comments:

Post a Comment