Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 6, 2014

Mwalimu ashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi

 
KILIMANJARO jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Muungano baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo.

Akitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari, kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,  Koka Moita alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 3 mwaka 2014, majira ya saa tano asubuhi katika mjini mdogo wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kamanda Moita alisema mwalimu huyo alifumaniwa na mwanafunzi huyo akifanya mapenzi katika nyumba ya kulala wageni iliyojulikana kwa jina la Kilimanjaro Gest House iliyopo katika eneo la Himo.

Akielezeea mazingira ya tukio hilo kamanda Moita alisema awali  mwalimu huyo alionekana akiwa amembeba mwanafunzi huyo katika pikipiki  ambapo alikuwa akielekea katika nyumba hiyo ya kulala wageni.

Kamanda alisema baada ya wazazi wa binti huyo kugundua kuwa mwalimu huyo alikuwa akimpeleka mwanafunzi huyo katika nyumba ya kulala wageni, walimfuatili na kumkuta akiwa chumbani na mwanafunzi huyo wakifanya mapenzi.
 
Aidha alisema mwalimu huyo anashiliwa katika kituo cha polisi Himo wilayani Moshi vijini, mkoani Kilimanjaro,  na kwamba taratibu za kisheri zitakapo kamilika atafikishwa mahakamani ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

No comments:

Post a Comment