Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 6, 2014

Wananchi wa mkoani Kilimanjaro walalamikia kukidhiri kwa uchafu hususani maeneo ya masoko



KILIMANJARO wananchi wanaoishi mkoani Kilimanjaro wanalalamikia kukithiri kwa uchafu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi  husani katika maeneo ya masoko jambo ambalo limechangia kushusha hadhi na sifa ya mji wa Moshi.

Mji wa Moshi ambao unajulikana kwa kuongoza kwa usafi nchini, mwaka huu ulishika nafasi ya pili hali ambayo wananchi hao walisema imechangiwa  na kukithiri kwa uchafu katika kila kona ya Mji huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwaandishi wa matandao huu wa "Kilimanjaro Officia Blog" mjini Moshi baadhi ya wananchi hao walisema hali ya uchafu katika maeneo mbalimbali ya mji Moshi inatisha ikilinganishwa na kipindi cha zaidi ya miaka minne iliyopita.

Kwa mujibu wa wananchi hao walisema soko Kuu la Mji wa Moshi lilifungwa na mamlaka ya chakula na dawa kutokana na uchafu uliokithiri katika maeneo mbalimbali ya ukuuzia vyakula jambo ambalo limekuwa likihatarisha afya za walaji.

Aidha walisema bado kumekuwa na mrundikano wa uchafu na maji machafu kutiririka katika masoko mengi huku halmashauri ya manispaa ya Moshi ikifumbia macho suala hilo na kuacha kuchukua taka hizo mara kwa mara.

Akizungumzia suala hilo  Kaimu Mkurugenzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Chirstoph Mtamakaya alikiri kuwepo kwa uchafu katika maeneo mbalimbali ya manipsaa ya Moshi kutokana na kufutwa kwa sheria ndogo ya mazingira.

Alisema kutokana hali ya uchafu kuendelea kukithiri halmashauri hiyo imejipanga kuteresha sheria hizo za usafi ili kuthibiti hali hiyo na hatima mji wa Moshi kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwa usafi nchini.

Alisema ujenzi wa soko kuu la Mjini Moshi lililofungwa kutokana na uchafu  na mamlaka ya chakula na dawa nchi TFDA limeshindikana kujengwa kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha .

Mtamakaya alisema manispaa hiyo imetenga zaidi ya shilingi milioni 278 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu na ukarabati  wa masoko ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko kuu la moshi.

No comments:

Post a Comment