Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 10, 2014

WANANCHI WAFUNGA CHUO KWA MAKUFULI KUPINGA CHUO HICHO KUUZWA KINYEMELA

KILIMANJARO wananchi wa kijiji cha Mshiri wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wameandamana na kuchukua uamuzi wa kufunga kwa makufukuli chuo cha ufundi Mshiri wakipinga chuo hicho kubinafsishwa kwa mwekezaji.

Wananchi hao walifikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa za kuaminika kwamba uongozi wa chuo hicho unataka kuuza chuo na kukabidhi kwa mwekezaji  bila ya kuwashirikisha wananchi.

Wakizungumza katika mkutano mkuu wa kijiji hicho uliofanyika juzi nje ya ofisi ya kijiji, baadhi ya wananchi hao Winford Mosha na Given Estomihi, walisema wanashangazwa na kitendo cha uongozi wa chuo hicho kutaka kubinafsisha chuo, huku uongozi huo ukifahamu fika  kwamba kilijengwa kwa nguvu za wananchi.

Walisema chuo hicho kilijengwa mwaka 1996 kwa michago ya wananchi, ambapo kila mwananchi alichanga shilingi 1000, huku wakishirikiana na mfadhili mmoja aliyejulikana kwa jina la Caty Allen na kwamba hawapo tayari kuona chuo hicho kikibinafsishwa kwa mwekezaji yeyote.
 
Walisema mapatano ya awali wakati wa makabidhino ya chuo hicho kwa mfadhili huyo, yalikuwa ni kukiendesha na iwapo itashindikana kukufanya hivyo akirudishe kwa serikali ya kijiji na sio kukibinafsisha au kukiuza  kama wanavyotaka kufanya.

Aidha walisema ni vema chuo hicho kikarudishwa kwenye mikono ya uongozi wa serikali ya kijiji, na kukiendesha wenyewe bila kuwepo kwa misaada ya mfadhili huyo, kutokana na kwamba hana nia njema na wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mshiri Wilson Mosha alisema maazimio waliofikia katika mkutano huo ni kuendelea kufunga chuo hicho mpaka pale muafaka utakapopatikana, na kwamba jambo hilo kwa sasa liko chini ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Moshi.

Aidha alisema ni vema serikali ikaiingilia kati suala hilo, kwani ni wazi linawakatisha tamaa wananchi kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo wanayoishi, kutokana na kwamba miradi hiyo imekuwa ikitumika ndivyo sivyo na kuwanufaisha watu wachache badala ya wajamii.

No comments:

Post a Comment