Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 10, 2014

Wilaya ya Siha yapatiwa msaada wa baiskeli 500 kutoka serikali ya Japan

KILIMANJARO halmashauri ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imepatiwa msaada wa baiskeli 500 kutoka serikali ya Japani  kwaajili ya kuwasaidia watoto yatima, walemavu  na wazee wasiojiweza ili waondokane na changamoto mbalimbali za kimaisha  ikiwemo chakula, mavazi, matibabu .

Naibu waziri wa tawala za mikoa na serikali  za mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni mbunge wa Siha Agrey Mwanri, aliyasema hayo wakati wa ghafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli hizo, yaliyofanywa na balozi mdogo katika ubalozi wa Japani, Bw. Kazuyoshi Matsunaga .

Mwanri alisema upatikanaji wa baiskeli hizo umetokana na mausiano mazuri, ya halmashuri hiyo na jiji la Ibaraki la nchini Japani na kwamba zitauzwa na fedha  zitakazo patikana zitatumika katika kusaidia jamii wakiwemo yatima, walemavu na  wazee, badala ya kuitegemea serikali  kufanya kila jambo.

Akikabidhi msaada huo balozi mdogo katika ubalozi wa Japani Bw. Kazuyoshi Matsunaga alisema baiskeli hizo ni sehemu tu ya misaada inayotarajiwa kuwasiliswa katika halmashauri hiyo na kwamba wanategemea misaada hiyo  italeta mabadiliko chanya katika halmashuri hiyo.

Kwa mujibu wa bwana Mwanri alisema, miradi mingine inayotarajiwa kutekelezwa kati ya jiji la Ibaraki na halmashauri ya Siha ni upandaji miti kwa kasi ambapo mradi huo utapatiwa  gari kwaajili ya kumwagilia maji  kipindi cha kiangazi, pia gari la wagonjwa kwaajili wa wananchi waishio pembezoni mwa wilaya hiyo, pamoja na gari la  zimamoto.

No comments:

Post a Comment