Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 24, 2014

Wananchi wavamia msitu wa asili na kuhatarisha vyanzo vya maji katika msitu huo



Wananchi wa kijiji cha makachaula wilayani Njombe wamevamia msitu wa asili nakuendesha shunguli za kiuchumi  kikiwemo kilimo hali ambayo inahatarisha vyanzo vya maji vinavyozunguka msitu huo.

Akizungumza na kituo hiki afisa mtendaji wa kata ya uwemba  chaazi kione katika mahojiano maalumu  amesema uharibifu mkubwa unatokana na shunguli za kilimo cha umwagiliaji  katika eneo la  msitu huo na kusema kuwa watu ambao wamebainika  watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha bw.kione amewataka wananchi wanaoishi jirani na msitu  huo kuendelea kushirikiana na serikali za vijiji vyao katika kuwabaini watu wanaokaidi agizo la serikali lakutokuendesha shunguli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji pamoja na uharibifu wa mazingira.

Mkoa wa njombe ni miongoni mwa mikoa iliyo na matukio mengi ya uharibifu wa  mazingira kutokana na shunguli za kilimo kwani   baadhi ya wananchi  huandaa mashamba kwa kuchoma moto.

Serikali kupitia sheria ya  utunzaji wa mazingira imepiga marufuku uharibifu wa mazingira na kutokuendesha shughuli zozote za kiuchumi kwenye vyanzo vya maji na kuwataka wananchi kuendesha shughuli hizo mita sitini kutoka kwenye vyanzo hivyo. 

No comments:

Post a Comment