Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 24, 2014

Wizara ya maliasili na utalii yaanzisha mfuko maalumu wa hifadhi ya mazingira

 
KILIMANJARO katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira  katika hifadhi za taifa, wizara ya maliasili na utalii imeanza mkakati wa kuanzisha mfuko maalumu wahifadhi wa mazingira, ambao ni endelevu kwaajili  huifadhi wa mlima Kilimanjaro na mlima meru  utakaotumika na jamii inayozunguka  milima hiyo kwa kuwapatia elimu  ya kulinda mfumo wa kiikolojia pia kuwawezesha kiuchumi.  

Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu, alisema  hayo mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro, kwenye kikao kilicho washirikisha baadhi ya wabunge na watendaji wa serikali, ambapo  alisema mfuko huo ni  maombi ya wabunge wa mkoa huo, na utatekelezwa na wizaza ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na wadau wa mazingira.

Alisema kila mwaka  Tanzania  inapoteza wastani wa hekta 375,000 za miti, na kwamba baada ya miaka 15 nchi inaweza kugeuka jangwa, hiyo niwajibu wa serikali kutafuta suluhisho kwa kukomboa mfumo wa kiikolojia , mfumo wa miti ,mfumo wa maisha na mfumo wa mito ambayo inatiririsha maji kutoka  tao la milima ya Kilimanjaro na Meru.

Naibu waziri tawala za mikoa na serikali za mitaa, ambaye pia ni mbunge wa Wilaya ya siha Aggrey Mwanri, amesema baada ya kuonauharibifu wa mazingira ikiendelea kwakasi karika hifadhi ya mlima kilimanjaro ,wabunge wa mkoa huo walipeleka kilio hicho serikalini ili kukpataufumbuzi wa tatizo hilo, ambalo lingeweza kuifanya nchi kugeuka jangwa.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya ardhi maliasili na mazingira  Abdulkarim Shah, alisema ili mpango  wa kuhifadhi mazingira uweze kuwa endelevu ni  muhimu kupeleka elimu ya utunzaji mazingira kwa kuanzia katika shule za msingi ili  wanafunzi waweze kutambua umuhimu wa kuyatunza mazingira.

No comments:

Post a Comment