Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 15, 2014

Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za ujambazi

 

KILIMANJARO watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wanashikiliwa na  jeshi la polisi  mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kupora kwa kutumia silaha za moto katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.Mbali na kushikiliwa kwa majambazi hao, pia  jeshi la polisi, limefanikiwa kukamata   bunduki mbili aina ya shotgun yenye namba za usajili 13704 ikiwa na risasi  tatu, pamoja bunduki aina ya SAR  yenye nambari 3811 ikiwa na risasi zake sita.Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Moita Koka, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao  na kusema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14 majira ya saa 04:00 usiku katika eneo la daraja la Holili tarafa ya Mengwe wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.Koka alisema watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi wamekuwa wakijihusisha na ujambazi wa kupora kwa kutumia silaha katika maeneo ya mbalimbali ya wilaya ya Rombo na Himo.Koka alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya askari kufanya msako mkali katika maeneo ya Holili kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha.Alisema askari hao waliwahoji watuhumiwa hao ambapo waliwaelekeza walipo  walipoficha silaha hizo na polisi kufanya upekuzi kwenye eneo hilo na kufanikiwa kukuta silaha mbalimbali ikiwemo bunduki hizo pamoja na mali mbalimbali walizo iba kwenye maduka ya watu.Aidha alisema jeshi la polisi linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao  kwa upelelzi zaidi na kwamba iwapo watakutwa na hatia watafikishwa mahakamani ili  sheria iweze kufuata mkondo wake.Koka ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuimarisha vikundi vya polisi jamii  katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuwa wepesi kutoa taarifa za siri za uhalifu kwa jeshi la polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema kabla ya madhara kutokea.


No comments:

Post a Comment