Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, November 4, 2014

Askari 84 wenye ulemavu wazuiwa kufanya mitihani yao ya mwisho katika Chuo Cha Polisi Moshi

KILIMANJARO serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi imeombwa  kuchunguza uongozi wa chuo cha polisi Moshi  ili kuondoa migogoro ya baadhi  askari wenye ulemavu na magonjwa ya kudumu walipelekwa chuoni hapo kusoma na   kupanda vyeo.

Hatua hiyo imekuja baada ya askari 84 waliofukuzwa na uongozi wa chuo hicho  kwaajili ya kushindwa kufanya mazoezi ya kijeshi kutokana na kuwa na magonjwa ya kudumu ikiwa ni pamoja na ulemavu waliopata wakiwa kazini kuendelea kuzuiwa kufanya mtihani wa mwisho licha ya agizo kutoka makao makuu ya jeshi hilo kutakiwa kurudishwa chuoni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakifanya mahojiano na waandishi wa habari, baadhi ya askari hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walisema wizara ya mambo ya ndani  nchi  ni vema ikafanya uchunguzi ili kubaini matatizo yaliopo chuoni hapo.

Walisema  uchunguzi huo utasaidia kuondoa migogoro ya upandaji wa vyeo kwa askari wenye ulemavu na magonjwa ya kudumu kwani uvunjifu wa haki za binadamu umekuwa ukifanywa na uongozi wa chuo hicho pasipo kujali wagonjwa.


Aidha walisema wamekuwa wakisoma masomo hayo ili kupanda vyeo na mishahara yao izidi kuboreshwa ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayo wakabili askari na kwamba serikali ni vema ikaangali sula hilo kwa maslahi ya askari wote.

Akijubu malalamiko hayo ya askari hao kuzuiwa kufanya mitihani hiyo Mkuu wa chuo hicho Matanga Mbushi alisema yeye hausiki na kurudishwa chuo kwa askari na kwamba suala la  kufanya mitihani makao makuu ndio watatoa maelekezo zaidi.

No comments:

Post a Comment