Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, November 4, 2014

Tatizo la maji katika manispaa ya Moshi itakua historia ifikapo mwezi Desemba mwaka 2014

KILIAMANJARO upungufu wa maji katika Manispaa ya Moshi linaekea kuwa historia ifikapo mwezi Desemba mwaka huu kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa  mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemchem ya Mto Karanga ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 382.

Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro, waliotembelea mradi huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ( MUWSA), Mhandisi Cyprian Luhemeja amefafanua kuwa, mradi huo utakapokamilika utahudumia maeneo ya Bomambuzi, Pasua , Matindigani na meneo ya katikati ya mji.

Mhandisi Luhemeja amesema maeneo hayo kwa sasa yana mgawo wa maji kutokana na uwepo wa maji kidogo ambapo pindi mradi huo utakapokamilika utawezesha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa saa 24.

Amesema mradi huo utasaidia kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa maji kwa mita za ujazo zipatazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa kusambazia maji ambapo kwa sasa umeshakamilika kwa asilimia 99.

Amefafanua kuwa gharama za mradi huo ni kubwa lakini gharama za uendeshaji ni ndogo kutokana na chanzo cha maji hayo kutoka katika chemchem ya mto karanga ambapo itasaidia upatikanaji wa maji saa 24.

Sambamba na hilo, Mamlaka hiyo imeiomba serikali kuwatumia watalamu wa ndani ya nchi katika masuala mbambali kwani imefanikiwa kutekeleza mpango wa matokeo makubwa kwa kutekeleza mradi mkubwa wa maji kwa kutumia wataalam wake wa ndani.

Kwa upande wake Mhandisi wa mradi huo Said Mrindoko,  amesema zipo changamoto mbalimbali ambazo walikumbana nazo wakati wa ujenzi wa mradi huo ikiwemo baadhi ya wananchi kujenga karibu na chanzo cha maji hivyo kusababisha kazi ya kulaza mabomba kuwa ngumu.

Mrindoko amesema pia wapo baadhi ya wananchi walikataa maeneo yao yasitumike katika ujenzi wa mradi hali iliyoilazimu mamlaka kuyanunua maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment