Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, November 13, 2014

Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii amewataka waongoza watalii "Tour Guides" kuhakikisha kuwa wana mikataba halali

KILIMANJARO Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mahmoud Mgimwa, amewataka waongoza watalii (Tour Guides) kuhakikisha kuwa wana mikataba halali ya kazi na wamiliki wa makampuni wanayofanyia kazi ili kuepuka kunyonywa haki zao.

Mgimwa ametoa rai hiyo wakati akitoa nasaha zake katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha waongoza watalii mlima Kilimanjaro (KGA) kilichofanyika mjini Moshi ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Respicius Baitwa alimwelezea waziri huyo kuwa, pamoja na ugumu wa kazi yao, baadhi ya wamiliki wa makapuni ya utalii wamekuwa wakiwanyonya haki zao.

Waziri huyo amewa ahidi waongoza watalii hao wa mlima Kilimanjaro kuwa, atakutana na chama cha wamiliki wa makapuni ya utalii nchini (TATO) pamoja na chama  cha wamiliki wa makampuni ya utalii Kilimanjaro (KIATO) ili kuona namna ya kulinda maslahi ya waongoza watalii hao.

Mgimwa amefafanua kuwa, hifadhi ya mlima Kilimanjaro ndio hifadhi ambayo inaaingizia serikali mapato makubwa ikilinganishwa na hifadhi nyingine hivyo kuwataka waongoza watalii hao kufanya kazi zao kwa umakini, uadilifu na nidhamu ya hali ya juu kwani kwa kutofanya hivyo watalikosesha taifa mapato makubwa yatokanayo na utalii.

Pia, waziri huyo amewataka wanachama wa KGA kuendeleza umoja wao ili waweze kusaidiana katika kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa vifaa maalumu vya kupandia mlima Kilimanjaro.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, Mwenyekiti wa chama cha waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro, Respicius Baitwa, ameiomba serikali kuingilia kati   viwango vya malipo vinavyotolewa na makapuni ya utalii, ili kukidhi  hali halisi ya kazi wanazozifanya za kuwaongoza watalii hao.

Amesema changamoto nyingine ni ukosefu wa vitendea kazi licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu ya kuwaongoza watalii hao.

Kwa upande wake mkuu wa mhifadhi ya KINAPA, Erasto Lufungulo, waongoza watalii wamekuwa sehemu  kubwa katika kuyatunza mazingira ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

Aidha ameongeza kuwa waongoza watalii wamekuwa wakitoa huduma bora, usalama wa wageni wenyewe hivyo kuwa sehemu ya watumishi wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment