Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, November 12, 2014

Wafanyakazi wa TANESCO mkoani kilimanjaro wapongezwa kwa kufikia malengo

KILIMANJARO serikali mkoani Kilimanjaro imewataka watumishi wa shirika la TANESCO, kufanya kazi kwa uadilifu ili kuzidisha ufanisi katika shirika hilo.

Hayo yalizungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, wakati wa sherehe za shirika hilo za kupongezana kwa kuvuka malengo ya kuwaunganishia umeme wateja wake mkoani Kilimanjaro.

Gama alisema TANESCO inaweza kufanikiwa  malengo yake kama watendaji kazi wake watakuwa waadilifu na  waaminifu , na kuongeza kuwa ni vigumu kupata mafanikio, kama watendaji hawata simama kwenye nafasi zao na kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Shirika la Umeme nchini (TANESCO),  Felschesmi  Mramba, amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kubadilika kiutendeji kazi hatua ambayo itawawezesha  kwenda na kasi ya mahitaji ya wateja ambao wanahitaji huduma hiyo.

Mramba alisema haiwezekani Tanzania ikawa nchi iliyoendelea kama wananchi wake wote hawatakuwa na huduma ya umeme.

Alisema mabadiliko ya kweli ni lazima yaanzie kwa watendaji wake, na kwamba shirika likibadilika litaibadilisha nchi, na tutakuwa na uchumi imara.

Aidha aliongeza kusema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la wateja ambapo katika miaka ya themanini walikuwepo wateja laki mbili tu lakini hadi kufikia mwaka huu 2014 wameongezeka na kufikia wateja 1.5.

No comments:

Post a Comment