Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, November 3, 2014

TFF watakiwa kutoka maofisini na kwenda kusaka vipaji vya michezo maeneo ya vijijini

KILIMANJARO viongozi wa shirikisho la soka nchini  TFF, wametakiwa kuondoka maofisini na kwenda kusaka vipaji vya michezo katika maeneo ya vijijini ambako kuna vipaji mbalimbali,  ili kuweza kuwapata wachezaji ambao watashiriki katika timu ya vijana ya taifa.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Vijana CCM, Ester Bulaya wakati alipokuwa akifunga mashindano ya John Samwel Malecela Cup 2014, ambayo yalishirikisha timu 16 za kata na timu 19 kutoka shule za sekondari zilizopo katika jimbo la Same Mashariki , ambapo mashindano hayo yaliandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela.

Mhe, Bulaya amesema mashindano hayo yametoa fursa kwa vijana kuibua vipaji vyao, na hivyo kutoa rai kwa Rais wa TFF, kuacha kuendelea kukaa ofisini na badala yake aende vijijini ambako kuna vipaji vingi vya wachezaji ambao ni vijana.

Bulaya amesema  viongozi wa TFF, wasikae ofisini, waende kutafuta vijana ambapo wataweza kushiriki kwenye timu za taifa za vijana, akili zao zisiishie kwenye timu za Simba na Yanga pekee.

Amesema TFF endepo kama wangekuwa wanatoka na kwenda kusaka vipaji vilivyopo katika maeneo ya vijiji wangeweza kupata wachezaji wazuri ambao wangeweza kuichezea timu ya taifa ya vijana na kuweza kuitangaza nchini katika medani za michezo.

Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na Mbunge wa jimbo  hilo  Anne Kilango Malecela, kwa lengo  la kuibua vipaji kwa vijana sanjari  na  kuwaelimisha vijana kujiepusha na vitendo viovu katika jamii  yameleta furaha kubwa kwa mashabiki wa timu hizo.

Kilango amesema "nia ni kuweza kuwaunganisha vijana wa jimbo langu ili kuibua vipaji walivyo navyo ili kupata wachezaji bora katika michezo mbalimbali."

Aidha katika michezo hiyo Mbunge huyo ametoa zawadi mbalimbali kwa timu zote zilizoshiriki michezo hiyo huku mshindi wa kwanza akiondoka na kitita cha shilingi laki saba na kombe.

Timu ya soka ya Maore ilifanikiwa kuchukua kombe hilo baada ya kuichapa timu ya Kihurio kwa goli 1-0 kwa  timu za Kata katika dimba la fainali lilochezwa katika viwanja  vya Mamba Myamba wilayani Same.

Katika upande wa timu za sekondari, timu ya Parane iliibuka mshindi katika fainali hiyo baada ya kuifunga timu ya  Ntenga sekondari Magori 2-0 na kuifanya timu ya Parane  kushika nafasi ya pili na kuzawadiwa kikombe na pesa taslimu kiasi cha shilingi  laki tano (500,000),huku timu ya Ntenga ikijinyakulia kikombe na pesa taslimu kiasi cha shilingi laki tatu (300,000).

No comments:

Post a Comment