Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 28, 2014

Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro umekama ng'ombe zaidi ya elfu kumi walioingia kwenye shamba la muwekezaji

KILIMANJARO, Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro wamekamata ng’ombe zaidi ya elfu kumi ambao wameingizwa kwenye shamba linalomilikiwa na mwekezaji Peter Jones, la Ndarakway,  lililoko kijiji cha Mitimirefu wilayani Siha mkoani hapa.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, amesema ng’ombe hao wamekamatwa wakitokea wilaya ya Longido, Siha na nchi jirani ya Kenya ambao waliingizwa na wafugaji wa jamii ya Kimaasai kinyume na taratibu.

Gama amesema tayari uongozi wa mkoa huo, umeongeza askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ili kukabiliana na kundi kubwa la  wafugaji hao ambao wameshindwa kutii amri ya serikali inayowazuia kuingiza mifugo katika eneo hilo la mwekezaji huyo.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa, ameongeza kusema kuwa  baada ya askari wa kutulisa ghasia kufika  katika eneo la mwekezaji huyo wafugaji  hao walitelekeza mifugo yao na kukimbilia mapori , na kwamba  Jeshi hilo linaendelea na msako mkali ili kuwakamata wamiliki wa mifugo hyo.
 
Amefafanua kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imeongeza nguvu kwa kuwapeleka askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), ili kukabiliana na wafugaji hao ambao licha ya kutoa amri inayowakataza kuingiza mifugo katika eneo hilo bado wafugaji hao wameshindwa kutii agizo hilo
Itakumbukwa kuwa novemba 21 mwaka huu wafugaji wa  jamii ya Kimaasai kutoka nchi jirani ya Kenya na wilaya ya Longido, walivamia shamba la mwekezaji huyo na kuteketeza nyumba kumi na sita na magari tisa wakidai eneo la malisho ya mifugo yao.

No comments:

Post a Comment