Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 28, 2014

Zoezi la ujenzi wa maabara lazidi kudorora katika wilaya za za Moshi Vijiji, Hai na Same mkoani Kilimanjaro

KILIMANJARO utekelezaji wa agizo la Rais la kuzitaka halmashauri za wilaya kujenga maabara za masomo ya katika shule za sekondari za kata nchini, limeoneka kusuasua katika wilaya za Moshi Vijiji, Hai na Same mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, aliyasema hayo jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya hali ya utekelezaji wa agizo hilo katika wilaya za mkoa wa Kilimanjaro.

Alisema ujenzi wa maabara katika shule za kata za wilaya hizo unaendelea kusuasua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo  muako mdogo wa wananchi wa uchangiaji wa fedha za ujenzi wa maabara katika maeneo  hayo.

Aidha alisema mpaka sasa zaidi ya maabara 497 zipo katika hatua za mwisho za ujenzi katika shule mbalimbali za mkoa wa Kilimanjaro na kwamba mahitahiji ya mkoani ni zaidi ya maabara 651.

Gama alisema zaidi ya shule  217 za sekondari za kata hazina maabara  na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wakutosha katika uchangiaji wa maabara ili kufanikisha malengo ya serikali ya kuinua ufaulu wa masomo ya Sayansi.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema ujenzi wa shule za sekondari  za vipaji maalumu katika masomo ya sayansi umekwisha kamilika katika wilaya zote na kwamba mwaka 2015 zitaanza kuchagua wanafunzi tayari kwa kuanza masomo.

Alisema shule hizo zitakuwa na kidato cha kwanza hadi kidato cha sita na ambapo zitakuwa ni za bweni na zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment