Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, December 2, 2014

Mama mjamzito ajifungulia barazani baada ya kunyimwa huduma katika kituo cha afya

KILIMANJARO wauguzi  wa zamu katika kituo cha Afya cha Pasua kilichopo Manispaa ya Moshi, wanatuhumiwa  kumtolea lugha chafu mama mjamzito ikiwamo pia kumnyima kitanda na hivyo kujifungulia nje ya baraza la nyumba ya jirani  muda mfupi baada ya kufukuzwa kituoni hapo.

Mama  huyo Josephine Michael (21), Mkazi wa kata ya Kaloleni, Manispa ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikumbwa na mkasa huo Novemba 29 mwaka huu, baada ya kufika kwenye kituo hicho kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kujifungua lakini katika hali isiyokuwa ya kiutu aliambulia kufukuzwa na wauguzi hao wa zamu.

Akizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog, Mama huyo amesema kuwa, baada ya kufika katika kituo hicho cha Afya,  majira ya saa mbili usiku na kuwaeleza wauguzi hao wa zamu  juu ya kile kilichokuwa kinamsibu, alielezwa kuwa hakuna kitanda kwa watu ambao si wagonjwa.

Amesema kuwa baada ya kuambulia majibu hayo, aliondoka na kurejea nyumbani kwake na alipofika nyumbani hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na hivyo kukimbilia kwa majirani kuomba msaada ambapo kabla ya kupatiwa msaada huo na majirani mfuko wa uzazi ulipasuka.

Miongoni mwa waliojitoa mhanga kuokoa uhai wa mama huyo pamoja na mtoto wake ni mwandishi wa habari, Safina Sarwatt (Mtanzania), ambaye alilazimika kutumia mwanga wa simu yake ya kiganjani kumzalisha mama huyo akishirikiana na majirani zake.

Sarwatt amesema licha ya kutokuwa na utaalamu wowote alijikuta katika wakati mgumu ingawa aliendelea kutoa msaada huo, na kumkimbiza katika kituo cha afya cha Pasua.

Akizungumza Mama huyo akiwa katika kituo cha afya cha Pasua wodi ya watoto amempongeza mwandishi huyo kwa kuwa na moyo wa kipekee  kwani ni watu wachache ambao wanaweza kujitolea.

Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Moshi, Shaaban Ntarambe hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo kwa kile alichodai suala hilo ni la kitaalamu na kuwataka waandishi wa habari kuandika maswali ili ayawasilishe kwa wataalamu wake wa Idara ya Afya.

No comments:

Post a Comment