Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, December 1, 2014

Mkuu wa shule ya msingi ampa ujauzito mwanafunzi wa shule ya sekondari


KILIMANJARO mwalimu mkuu wa shule ya msingi iliyopo wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro (jina tunalihifadhi) anatuhumiwa kumtia mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Boon, mwenye umri wa miaka 17.

Mwalimu huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama alimpa ujauzito binti huyo na kupelekea uongozi wa shule hiyo kumfukuza shule kwa mujibu wa kanuni na sheria za kiserikali.

Akizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog jana katika mahojiano maalumu
Mkuu wa shule ya sekeondari ya Boon anaposoma binti huyo aliyepewa uja uzito.  Mwalimu mkuu huyo alikiri kweli mwanafunzi huyo ni mjamzito na mimba hiyo ni ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi iliyopo wilayani Rombo.

Shirima alisema mwanafunzi huyo alibainika akiwa na jauzito huo Novemba 25 mwaka huu baada ya ugomvi mkubwa kuzuka shuleni hapo baina ya mwanafunzi huyo na mwanafunzi mwingine wakimgombea mwalimu mkuu huyo aliyempa ujauzito.

Alisema baada ya ugomvi huo ndipo mwanafunzi mmoja alitoka na kwenda kwa mwalimu wa malenzi na kumweleza suala hilo na ndipo uongozi wa shule ulichukua hatua ya kwenda na kumpima binti huyo ambapo alibainika anaujauzito wa mienzi nne.

Alisema baada ya vipimo kuthibitisha mwanafunzi huyo ni mjamzito uongozi wa shule hiyo ulitoa taarifa katika kituo cha polisi Mengwe na jambo lililofanikisha mwalimu huyo kushikiliwa kwa maojiano zaidi.

Aidha alisema baada ya hatua hiyo alitoa taarifa pia kwa mtendaji wa kijiji na diwani wa kata hiyo ambapo wazazi wake walitaarifiwa na kukabidhiwa mtoto wao mbele ya viongozi hao.

Alisema changamoto kubwa inayo wakabili ni wazazi kufanya siri na kuficha matukio hayo pamoja na jitihada zinazofanyika katika kutokomeza mimba mashuleni.

Mwalimu huyo alisema tukio hilo ni tukio la pili la walimu kuwapa mimba wanafunzi na kwamba wamekuwa wakisikitishwa na hatua zinazochukuliwa kutokana na mmoja wa mwalimu aliyetenda kosa hilo kuendelea kufundisha na kuzurura mitaani na hakuna hatua yeyote aliyochukuliwa dhidi ya kosa alilotenda la kumpa mwanafunzi ujauzito.

Shirima alisema wazazi wamekuwa wakichangia vitendo vya kuporomoka kwa maadili ya watoto kutokana na kuwakabidhi simu ambazo wamekuwa wakiwasiliana na wanaume na kupeleka kupata ujauzito na kupoteza sifa ya kuendelea na masomo.

Aidha alisema watoto wengi wamekuwa wakiishi na bibi zao hivyo kushindwa kupata malezi bora kutoka kwa wazazi wao binafsi huku walezi wengine wakiwa kwenye shuhuli zao za kutafuta pesa na kusau wajibu wa malezi ya watoto.

No comments:

Post a Comment