Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, January 31, 2015

Ashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuchoma nyumba

KILIMANJARO JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la John Macha, kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya jirani yake kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya jirani huyo kudaiwa kuhusika katika mauaji ya ndugu yake Faustine Macha.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mkoani Kilimanjaro, Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:00 subuhi januari 29 mwaka huu katika kijiji cha kanango wilayani Moshi vijijini.

Alisema afisa mtendaji wa kijiji hicho Kamilius Kessy (56) alibaini kuwa nyumba hiyo ilikuwa inateketea kwa moto  baada ya kuchomwa na mtuhumiwa kwa kile alichokua anadai analipiza kisasi kutokana na mwenye nyumba huyo kuhusika katika mauaji ya ndugu yake.

Mwenye nyumba huyo anadaiwa kufanya na kushiriki katika mauaji ya  ndugu yake aitwaye Faustine  Macha kwa kumpiga na rungu kichwani na kisha kumshambulia kwa kipigo sehemu mbalimbali za mwili wake jambo lililo sababisha kifo chake januari 28 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi.

Kamanda alisema nyumba hiyo iliyokuwa imejengwa kwa matofali ya udongo na kuezekwa kwa makuti iliteketea na mali zote zilizokuwepo ndani ya nyumba na kwamba thamani halisi ya mali iliyo teketea bado haijajulikana mpaka sasa.

Aidha alisema tukio hilo limefanyika wakati mwenye nyumba huyo akiwa ametoroka kusiko julikana kutokana na tuhuma za mauaji  zinazo mkabili na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio.

Alisema tukio hilo halijasababisha madhara yoyote kwa binadamu na kwamba mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment