Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, January 28, 2015

Habari njema kwa wafanyabiashara na wateja wa soko la mboga na matunda Uchira

KILIMANJARO  halmashauri ya wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, inakusudia kuanza ujenzi wa choo kwenye soko la mboga na matunda, inalotumiwa na wafanyabiashara pamoja na wanunuzi katika eneo la Uchira wilayani hapa.

Ujenzi wa choo hicho unatarajiwa kuanza mwezi Februari mwaka huu, baada ya halmashauri hiyo kufanya makadirio ya ujenzi na gharama halisi za kutekeleza mradi huo, ambao ni muhimu kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.

Akizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu wa Kilimanjaro Oficial Blog ofisini kwake, mkurugenzi wa halmashauri hiyo Fulgence Mponji, alisema kuwa kukwama kwa ujenzi wa choo hicho kulitokana na makadirio ya mhandisi wa halmashauri kuzidi gharama zilizowekwa kwenye bajeti ya utekelezaji.

Hata hivyo amefafanua kuwa makadirio ya ujenzi yaliyotolewa na mhandisi wa halmashauri hiyo yalionesha ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni sita, juu ya fedha zilizotengwa kiasi cha shilingi milioni tano.

Awali watumiaji wa soko hilo la Uchira, walilalamikia ukosefu wa choo, hivyo kuwaweka kwenye hatari ya kupatwa na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko.

Wafanyabiashara hao walisema soko hilo ambalo pia linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji, imewalazimu wafanyabiashara kujisaidia kwenye mifuko ya rambo na kuitupa hovyo.

Changamoto hizo zilizodumu kwa zaidi ya miaka kumi sasa imeendelea kuwa kero kwa watumiaji wa soko hilo, ambao wamelalamikia kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu licha ya kuwepo wakala aliyepewa zabuni ya kukusanya ushuru bila kupata huduma hizo muhimu za kijamii.

No comments:

Post a Comment