Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, January 28, 2015

Viongozi wa ngazi za vijiji wilayani Hai waonywa kuacha kuendeleza migogoro ya arthi

KILIMANJARO serikali imewaonya viongozi wa ngazi za vijiji wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kuacha tabia ya kuendeleza migogoro ya ardhi inayoendelea kushamiri wilayani humo badala yake watumie nafasi walizonazo kuitatua ili kuepusha vurugu zisizo za lazima kwa wananchi.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga, wakati akizungumza na wananchi  kwenye mkutano wa kawaida wa kuwaingiza kazini wenyeviti  wapya wa vitongoji  waliochaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa katika kijiji cha Foo  wilayani humo.

Makunga alisema kumekuwa na baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali za vijiji ambao huchochea migogoro ya ardhi ambayo haina tija wala maslahi kwa serikali bali imekuwa ikigharimu maisha ya watu na kwamba nivema sasa viongozi hao wakalenga kuitatua zaidi.


Aidha Makunga aliwataka viongozi hao kusimamia na kutekeleza dhana ya utawala bora ili kuleta ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao, ikiwa ni pamoja na kuweka itikadi za kisasa pembeni ili kufanyakazi ya kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.

 Aliendelea kusema kuwa ni vema viongozi na wananchi kuwa na tabia ya kusimamia miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao ili kuthibiti baadhi ya watu  wenyenia mbaya ya  kuchakachua  miradi hiyo.

Alisema wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamekuwa wakisuasua kusimamia miradi ya maendeleo ya vijana katika maeneo yao jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa wingi wa vijana kuzuruza na kukaa vijiweni kutokana na  kukosa kazi za kufanya huku kukiwa na frusa nyingi za kuwakomboa kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Foo Judica Mmasi, alisema kijiji hicho kimekuwa kikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu miundombinu ya  barabara jambo ambalo limekuwa likisababisha kutopitika kirahisi wakati wananchi wakiende kufuata huduma muhimu kama afya.

No comments:

Post a Comment