Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, January 20, 2015

Kilimanjaro FC yajihakikishia ubingwa kabla ya ligi kumalizika

KILIMANJARO, Klabu ya Kilimanjaro FC yenye makazi yake Pasua, inayocheza ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa Kilimanjaro imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kuifunga Afro Boys ya majengo, goli 1 kwa sifuri.

Mchezo huo wa raundi ya pili ulichezwa tarehe 18 Januari 2015 katika kiwanza cha Ushirika mjini Moshi, ikiwa ni hatua ya sita bora. Ambapo timu ya Kilimanjaro FC iliibuka kidede baada ya mchezaji wao
Jackson Obadia "Messi" kuunganisha pasi mpira wa pasi uliotoka kwa Ayubu
Lipati
katika dakika ya 48 kipindi cha pili.

Kwa ushindi walioupata Kilimanjaro FC, sasa timu hiyo inahitaji kushinda mchezo mmoja tu kati ya michezo yake miwili iliyobaki ili kutangazwa kuwa bingwa wa msimu wa 2014/2015 mkoani Kilimanjaro.

Mpaka sasa
Kilimanjaro FC, imeshajikusanyia Pointi 19, ambapo inahitaji kushinda mchezo mmoja tu ili kufikisha pointi 22 ambazo hamna timu yoyote inayoweza kufikia pointi hizo.

Msimamo wa ligi hiyo unaotarajiwa kumalizika, Februari mosi mwaka 2015, unaonesha kuwa Kilimanjaro FC inaongoza kwa pointi 19, ikifuatiwa na Hai City, yenye pointi 15 sawa na Afro Boys, iliyoko katika nafasi ya tatu, zikizidiana kwa tofauti ya magoli.

Nafasi ya nne ni Polisi Mwanga, yenye pointi 13 na mchezo mmoja mkononi, nafasi ya tano ni Polisi Kilimanjaro, yenye pointi 4 huku Sango FC, isiyokuwa na Pointi hata moja ikishikilia mkia.

No comments:

Post a Comment