Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, January 20, 2015

Ofisi ya mkuu wa mkoa Kilimanjaro yatuhumiwa kushiriki kupora maeneo ya uwekezaji

KILIMANJARO, mstahiki meya wa halimashauri ya manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro Jafary Michael, ameilalamikia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, kutokana na kushiriki katika uporwaji wa maeneo ya uwekezaji kwa maslahi binafsi ya baadhi ya watu binafsi.

Akizungumza na vyombo vya habari jana mjini Moshi, Jafari alisema kumekuwa na jitihada za baadhi ya watu kutaka kupora eneo la uwekezaji lenye thamani ya shilingi milioni 700 hadi bilioni moja lililopo katika kata ya Mawenzi karibu na jingo la ofisi za makao makuu ya polisi mjini Moshi.

Jafary alisema katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Severni Kahitwa, aliandika barua ya kumuagiza Mkurugenzi wa halmshauri hiyo Shaabani Ntarambe, kuhakikisha kwamba hati ya eneo hilo inatengenezwa haraka kwa jina ya kikundi ambacho kinataka kupora eneo hilo.

Alisema kikundi cha watu hao kimekuwa kikisaidiwa na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na baadhi ya watendaji wa halamshauri ya manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanasiasa pamoja na wadau wengine wenye maslahi binafsi na eneo hilo.

Aidha alisema halmashauri hiyo ilipata haki ya kuhodhi eneo hilo kama mali ya serikali kwaajili ya matumizi ya umma kupitia taratibu mbalimbali za kikanuni, kimiongozo na kisheria na kwamba eneo hilo limepangishwa kwa wafanyabishara ambao wanachangia pato la ndani la halmashauri.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya mipango miji na arthi katika manispaa ya Moshi Alex Poteka, alisema kiwanja hicho hapo awali kilikuwa kikimiliwa na kikundi kiitwacho Mawenzi Sport clab na kwamba hatimiliki yao ilikwisha muda wake mwaka 1973 ambapo eneo hilo lilirudi na kuwa mali ya halmshauri hiyo.

Alisema wakati halmashauri hiyo ikiendelea na mawasiliano na kamishna msaidizi wa arthi kanda ya kaskazini kwaajili ya kutengeneza hatimiliki ya eneo hilo ndipo kikundi hicho kiliibuka na kulidai eneo hilo tena wakitaka kugushi hati yao iliyokwisha muda wake jambo ambalo lilipelekea mgongano kati ya kikundi hicho na halmashauri hiyo.

Hata hivyo mkurugenzi wa Manispaa hiyo Shaabani Ntarambe, alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya ukweli wa kuwepo kwa barua ya maagizo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa mkoa Kilimanjaro ya kumtaka kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hatimiliki ya kikundi hicho alisema kwasasa wao wanafuata muongozo kutoka katika ofisi ya kamishna msaidizi wa ardhi kanda ya kasikazini.

Akizungumzia juu ya tuhuma hizo za kuandika barua ya maagizo hayo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro alisema Severni Kaitwa, alisema kuandika barua ya magizo hao sio kawaida na kwamba utawatibu haupo hivyo.

No comments:

Post a Comment