Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, January 30, 2015

Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo akinzana na wabunge wa UKAWA

KILIMANJARO mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), ametoa kauli inayokinzani na viongozi wa UKAWA, kwa kulitaka Jeshi la Polisi nchini liendelee kufanya kazi yake ya kuwapiga raia.

Kauli hiyo aliitoa  leo ofisini kwake Mjini Moshi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa, haoni sababu ya viongozi wa Ukawa kuwalaumi Jeshi la Polisi kwa kuwapiga raia.

Ndesamburo alisema kuwa, kwa sasa wananchi wanahitaji mabadiliko, huku Jeshi la Polisi nalo likiwa limechoka, hivyo limekuwa likifanya ukatili wa kuwapiga raia ili kuwapa hasira na Serikali yao, na kufanya mabadiliko.

 “Kitendo  cha Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi, ni kitendo cha kuwafanya wawape hasira na Serikali iliyopo madarakani, na kuamua kufanya mabadiliko, hivyo viongozi wa UKAWA tunapaswa kuwaunga mkono Jeshi letu la polisi, kwani linasaidia vyama vya upinzani kuing'oa CCM” alisema Ndesamburo.

Alisema Vyama vya upinzani vimekuwa vikitumia siasa ya ustaarabu kwa muda mrefu bila ya mabadiliko yoyote, huku viongozi wa CCM wakiwa wanawanyanyasa wananchi, sasa imefika wakati ambapo mabadiliko yanahitajika.

Katika kikao cha Bunge kilichofanyika juzi, baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani, wanaounda UKAWA, walilaumu kitendo cha Jeshi la Polisi nchini, kuwapiga raia wasio kuwa na hatia.

Sakata hili la Jeshi la Polisi kupiga raia, lilifika bungeni baada ya kupigwa na kudhalilishwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba na wafuasi wengine wa chama hicho.

Katika sakata hilo, wabunge wa vyama vya Upinzani, walitaka awajibishwe Waziri mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, Naibu wake (DIGP), Abdukrahman Kaniki, pamoja na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Paul Chagonja.

Wabunge wa kambi ya Upinzani Bungeni, walitoa hoja kwa nyakati tofauti, wakati wakichangia mjadala kuhusu hoja iliyohusu jambo la dharura, iliyotolewa na Mbunge wa kuteuliwa (NCCR- Mageuzi), James Mbatia, na kauli ya Serikali kuhusiana na yaliyotokea Januari 27, mwaka hu, Mbagala jijini Dar es salaam.
 
Na Queen Isack

No comments:

Post a Comment