Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, January 19, 2015

Mwenyekiti wa Sanya Hoyee amewataka wenyeviti wa vitongoji kuimarisha ulinzi shirikishi

Kilimanjaro mwenyekiti wa Kijiji cha Sanya Hoyee Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro Moses Munuo amewataka Wenyeviti wa Vitongoji Katika Kijiji hicho kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao ili kupunguza matukio ya kihalifu ambayo yameongezeka kwa wingi yakiwamo wezi wa kuku na magodoro.

Mwenyekiti huyo alitoa wito huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kuongezeka matukio ya kihalifu katika kijiji hicho jambo ambalo linarudisha  maendeleo ya wananchi nyuma.

Munuo alisema hivi karibuni katika nyumba inayomilikiwa  na  Neema Omari iliibiwa vitu mbalimbali ikiwamo redio, godoro, kuku 14 na fedha taslimu ambazo hazija julikana idadi yake.

Ambapo alisema watu wawili wanefikishwa kwenye Ofisi yake mmoja kukutwa na godoro ambapo anafahamika kwa jijna la mama Sara mkazi wa Sanya hoyee na mwingine alikuwa mwenyekiti mstafu Jastin Kess  wa kitongoji cha makao mapya ambapo alikutwa na kuku wa nne.

Na watuhumiwa walipohojiwa wapi walikozitoa hizo mali mama Sara alisema kuwa yeye alipewa na mwenamke mmoja anayafahamika kwa jina la Happy Tenga, na alipotafutwa Happy na kuulizwa kuhusu tuhuma zinazomkabili za kumpa mama Sara godoro alikana na na kutaka jambo hilo lifikishwa katika kituo cha polisi Sanya juu.

Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu yeye alisema kuwa kuku hao amewanunua kwa kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Marwa Chacha na walipofika  nyumbani kwa kijana huyo alikimbia ndipo wananchi walipotaka kuchoma nyumba ya kijana huyo kwa kuwa ndiyo amekuwa akiwasumbua kwa wizi wa kuku ambapo polisi walifika na kuzuia.

Mwenyekiti huyo alisema vikundi hivyo shirikishi vinatakiwa kuundwa na wenyeji na kwamba vitasaidia kuwatambua wahalifu na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment