Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, January 19, 2015

Shilingi bilioni mbili zatumika kujenga barabara katika wilaya ya Same

Kilimanjaro kiasi cha Shilingi bilioni 2 kimetumika kukamilisha ujenzi wa barabara katika vijiji vya Mamba Myamba na Mpinji  vilivyopo katika Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro huku wananchi wa kipongeza hatua hiyo.

Wakizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog, wamesema tangu nchi ipate Uhuru mwaka 1961 walikuwa wakiteseka kutokana na kukosekana kwa huduma mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara.

Mmoja wa wakazi wa Mamba Myamba, Elieti Kikoro alisema walikuwa wakilazimika kubeba mizigo yao kichwani au kwa kutumia wanyama kama punda kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu hususani kipindi cha masika.
Alisema kujengwa kwa barabara hizo kumekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi waishio milimani katika jimbo hilo ambalo hawakutegemea kama siku moja watakuwa na barabara ambayo itawezesha kusafirisha mazao yao.

Diwani wa Kata ya Mamba Myamba, Michael Chikira alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kufungua fursa za kiuchumi na wananchi wataweza kuzalisha kwa wingi zao lao la tangawizi na kuinua pato la taifa. Alisema barabara hiyo ilianza kujengwa kufuatia ombi lililotolewa kwa Rais Kikwete na Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela, ambao Rais Kikwete aliahidi kutekeleza ombi hilo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango Malecela, alisema kujengwa kwa barabara hizo ni msaada mkubwa kwa wananchi waishio maeneo ya milimani katika jimbo hilo. Aidha Kilango aliongeza kuwa barabara hizo zenye urefu wa Kilometa 13.8,  zimegharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili, na kwamba maeneo zilizopojengwa barabara hizo ni barabara ya Parame Kitubwa-Korogwe Mpinji (Km 8.7), na Kiwandani Manga-Chalinze (Km 4.8).

No comments:

Post a Comment