Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, January 26, 2015

Sakata la kuwepo njama za kuporwa kwa kiwanja cha Mawenzi lachukua sura mpya

KILIMANJARO sakata la kiwanja cha Mawenzi, kilichopo kata ya Mawenzi manispaa ya Moshi, limechukua sura mpya, baada ya Madiwani wa CHADEMA kuomba kuitishwa kwa kikao maalumu, kwa lengo la kujadili sakata hilo na kulitafutia ufumbuzi.

Kikao hicho Maalumu cha Baraza la Madiwani, kililazimika kugeuka kuwa kamati, kutokana na kuonekana kuwepo kwa tuhuma dhidi ya mkurugenzi wa Manispaa hiyo Shabaan Ntarambe kuhusiana na uporwaji wa  kiwanja hicho.

Akifungua kikao  Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Jafary Michael, alisema lengo la kikao hicho ni kujadili Hatma ya kiwanja hicho, ili kuwaeleza  wananchi ukweli kuhusiana na mmiliki halali wa eneo hilo.

Alisema ni vema Madiwani wakaweka itikadi za kisiasa pembeni, kutokana na kwamba wote wamepewa dhamana ya kusimamia na kulinda mali za wananchi.

Aidha Meya alielezea kusikitishwa kwake, na  uwepo wa hisia za vurugu katika kikao hicho, hali iliyosababisha kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya usalama, wakiwemo askari kanzu, walionekana kurandaranda katika eneo la Manispaa, wakiimarisha ulinzi, huku wakiwa hawajavaa  sare.

No comments:

Post a Comment