Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, January 26, 2015

Watu watano wakiwemo masister wawili wanusurika kufa katika ajali

KILIMANJARO watu watano wanusurika kifo baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana wilayani hai mkoani kilimanjaro.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 asubuhi katika barabara kuu ya sanya juu bomang'ombe eneo la zafanana.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliona gari likiwa kwenye mwendo kasi na kutaka kumpita gari lingine ambapo lilishindwa  kupita na kuligonga gari hilo kwa nyuma na kusababisha magari hayo kupinduka.

Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni aina ya suzuki yenye nambari za usajili T245 ADL, lililokuwa likiendeshwa na dereva anayefahamika kwa jina la Azizi Nasoro, makazi wa bomang'mbe ambaye ndiye mmiliki wa gari hilo ambalo ndiyo lililosababisha ajali hiyo.

Gari jingine ni aina ya Toyota Landcuser lenye nambari za usajili T778 ATL, mali ya Masister wa Gezeulole Bomang'mbe lilikuwa likiendeshwa na Sister Anna Matarimo, ambapo walikuwa wakitokea katika kanisa RC bomang'mbe kuelekea Gezaulole wanakoishi.

Mganga wa zamu anayejitambulisha kwa jina la Dk. Anjelista Shirima, alithibitisha kupokea majeruhi watano katika hospitali ya wilaya ya hai mkoani Kilimanjaro na kwamba kati ya majeruhi hao watatu wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu, na wawili ambao ni Masistar wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC moshi, ambao ni sister Anna matarino na Sister Terezi Olonyo, na walioruhusiwa ni Azizi Nasoro, Belda Matolo na Joseph Romwal.
 
Juhudi za kumtafuta kamanda wa mkoa kuzungumzia tukio hili ziligonga mwamba.

No comments:

Post a Comment