Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, February 19, 2015

Binti wa umri kati ya miaka 15-16 aliyeishi kwa takribani miaka 10 kwenye shina la mgomba

KILIMANJARO binti mwenye ulemavu wa akili anaye kadiriwa kuwa na umri kati ya miaka kumi na tano na kumi na sita amegundulika kuwa akifungiwa kwenye shina la mgomba na kisha kamba kufungwa kwenye mti uliopo karibu kwa muda wa miaka  10.

Tukio hili litokea katika  kijiji cha Narumu Tela wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambapo timu ya dawati la jinsia na watoto wiliya ya Hai walipo kwenda kijijini hapa kwa lengo la kuitembelea familia ya mwanamke mmoja aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia.

Kwa mujibu wa baba mdogo wa binti huyo Mr. Korenti Willium  Ngowi(37) mkulima na mkazi wa Narumu Tela, wazazi wa binti huyo walitengana wakiwa wadogo yeye na dada yake kabla baba yao hajafariki walikuwa chini ya uangalizi wa bibi yao Antonia Willium Ngowi aliwalea na baba yao Beatus Willium Ngowi  alipofariki waliendelea kulelewa na bibi  huyo.

Ngowi anasema kuwa baada ya muda binti huyo aliugua degedege akiwa katika umri mdogo hivyo alikuwa na tabia ya kukimbia nyumbani ndio bibi huyo akanza kumficha na  baadae kuanza kumfungia katika shina la mgomba na kamba kufungiwa katika mti uliopo karibu na mgomba huo.

Usiku alikuwa anawekwa katika zizi la ng`ombe analala huko na asubui anatolewa na kufungiwa katika shina hiyo kila siku  ndiyo yalikuwa maisha yake na bibi yake akiendelea na shunguli zake za kila siku alisema Ngowi.

Anasema kuwa  kwa sasa jukumu la kumuhudumia mtoto huyo na familia nzima limeachwa kwa mdogo wao wa mwisho Protesi Willium Ngowi anaye ishi kijiji cha Orori Narumu huwa anakuja asubui  kulisha ng`ombe na kumfungua binti huyo kutoka kwenye zizi  hilo na kuendelea kumfunga katika shina.

Alisema Majukumu yote yameachwa kwa Protesi kwani bibi ya binti huyo kwa sasa yupo dar es salaam kuhudhuria harusi  ya mmoja wa wajukuu zake.

Binti huyo kwa muda wote amekuwa hawasiliani na mtu yeyote isipokuwa wanafamilia wanaomhudumia ambapo  kutokana na hali hiyo amekuwa hawezi kumtazama mtu yeyeto usoni anaficha uso wake.

Pembeni ya binti alipokuwa amefungwa palikua na vyakula vya siku zilizopita ikiashiria kwamba hakuna mtu wa kumwangalia kama amekula au la, na pia palikuwa na chungu. 

Kwa mujibu wa majirani walisema kuwa chungu hicho huwekwa pembeni ya binti huyo kila siku akipelekwa ndani na chungu hicho pia hupelekwa ndani.

 Binti huyo ambaye alikuwa  haongei kwa kuogopa  watu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa polisi na baba yake mdogo Mr. Korenti Willium  Ngowi ameshikiliwa na polisi huku wakisubiria bibi huyo kurudi kutoka safarini.

No comments:

Post a Comment