Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, February 19, 2015

Kesi inayomkabili mkurugenzi wa manispaa ya Moshi dhidi ya wafanyabiashara wa mananasi yanguruma leo

KILIMANJARO mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi imejipanga kuanza kusikiliza kesi  dhidi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Shabaan Mtarimbe na wafanyabiashara wa mananasi mapema 23 febuari mwaka huu.

Uamuzi huo wa kusikilizwa umepatikana baada ya  mwanasheria wa  upande wa mlalamikiwa  Silivia Shayo, kuomba hahakama hiyo kutoa nafasi ya  upande huo kusikilizwa .

Alisema, haki ya kujieleza na kusikilizwa kwa pande zote mbili ni haki ya kila mtanzania na ni democrasia ya kweli, hivyo ameitaka mahakama kutoa nafasi ya manispaa hiyo kujitetea  kabla ya hukumu.

“Kesi hii ilisikilizwa upande mmoja tu, hivyo tunaiomba mahakama hii tukufu kutupa nafasi ya kujieleza kabla ya kutoa uamuzi mdogo wa mahakama”

Naye mwanasheria wa serekali  David Shilatu, alisema,  “Mahakama hii tukufu, lazima iangalie hali ya wafanyabiashara hao wadogo wanaoteseka na kutaabika kutokana na mali zilizotiwa mbaroni kuwa ndio tegemeo la familia zao na ndizo zinazosaidia  maisha ya kila siku  pamoja na familia zao.

Nae hakiimu Julieth Mahole alihairisha kesi hiyoo hadi Februari 23 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment