Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 7, 2015

Bunge laitupilia mbali hoja ya Mheshimiwa Kafulila ya kuitaka serikali kuwakilisha ripoti ya TAKUKURU bungeni

DODOMA bunge limeikataa hoja binafsi  ya mbunge wa Kigoma  Kusini mheshimiwa DAVID KAFULILA ya kuitaka serikali iwasilishe  bungeni ripoti ya Taasisi  ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kuhusu uchunguzi wa tuhuma za rushwa katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
 
Kwa mujibu wa barua iliyotoka ofisi ya bunge kwenda kwa mheshimiwa KAFULILA inasema  hakuna ibara yoyote ya Katiba wala kifungu chochote cha sheria kinacholipa bunge madaraka ya kuitaka serikali iwasilishe bungeni ripoti yoyote ya kiuchunguzi ya TAKUKURU ili ijadiliwe bungeni.
 
Aidha suala hilo lilishajadiliwa na kuhitimishwa na bunge katika mkutano uliopita na bunge lilishatia maazimio yanayotakiwa kutekelezwa na serikali na TAKUKURU.
 
Pia katika barua hiyo inasema kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 54 kifungu kidogo cha 4 ya kanuni za bunge inasema hoja yenye lengo la kutaka kujadili jambo lililokwisha amuliwa na bunge katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kabla ya kikao kinachoendelea ifikiriwe tena na haikubaliki labda kama ni hoja ya kutaka uamuzi huo wa bunge uliokwisha fanyika ubadilishwe.
 
Akizungumza  na waandishi wa habari leo mjini Dodoma mheshimiwa KAFULILA amesema katika bunge lililopita walichojadili na kufanya maamuzi ni kuhusiana na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) kuhusiana na Escrow na sio kuhusiana na taarifa ya TAKUKURU.

No comments:

Post a Comment