Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 7, 2015

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Hai atoa siku saba kwa viongozi wa serikali za mitaa waliokataa kuapishwa

KILIMANJARO mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Meleckzedeck Humbe  ametoa siku saba kwa viongozi wa serikali za mitaa kutoa maelezo ya kukaidi agizo la serikali la kuapishwa kabla ya kufanya kazi la sivyo nafasi hizo zitakuwa wazi.

Humbe ametoa agizo hilo katika ukumbi wa halmashauri ya Hai wakati akiwaapisha viongozi wa vijiji waliosalia ambapo kati yao waliapishwa 63 waliohudhuria baada ya viongozi 133  ambao 70 hawakuweza kuhudhuria  kabisa kwa ajili ya kuapishwa na kuanza kazi rasmi.

''Nitatoa siku saba kwa vingozi ambao wamekaidi agizo hili la serikali kuwa ni wajibu wa kila kiongozi kuapishwa kabla ya kuanza kazi  waandike maelezo ndani ya siku hizi saba kimaandishi kwa nini hawataki kuapishwa ili tujue nafasi hizo zipo wazi kwa uchaguzi mwingine'' alisema Humbe.

Humbe  aliongeza kuwa ni sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mtaa kiongozi yeyote kula kiapo kabla ya kuanza majukumu yake ya uongozi na kwa yule ambaye atakiuka kanuni na sheria hizo endapo atabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Hata hivyo humbe ameongeza kuwa viongozi waliochaguliwa wasimamie sheria na kanuni za serikali za vijiji na kuacha malumbano katika kipindi cha utendaji wa kazi.

No comments:

Post a Comment