Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 21, 2015

Jamii imeshauriwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu

KILIMANJARO jamii imeshauriwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu na wenye utindio wa Ubongo na badala yake wa wapatie huduma muhimu sawa na wasio na ulemavu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kikundi kinachojihusisha na kuwapitia  Elimu wanawake walemavu na watoto kiitwacho Songambele kilichopo mkoani Kilimanjaro na Arusha, Faustina Urasa.

Urasa alitoa kauli hiyo alipotembelea kituo kinacholelea watoto wenye mtindio wa ubongo cha Gabriella, kilichopo mjini Moshi, na kutoa sare za nguo kwa ajili ya kujifundishia mapishi, ambapo mafunzo hutolewa kituoni hapo.

Alisema kuwa, jamii imekuwa haiwathamini watoto wenye ulemavu mbalimbali ikiwemo mtindio wa ubongo huku wengine wakifikiria imani za kishirikina na kuwafungia ndani huku wengine wakiwanyanyapaa wakinamama wanaojifungua watoto wenye ulemavu.

“Watu wamekuwa wakiwanyima haki za msingi watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu au mtindio wa ubongo, na kuwafanya kutokupata mahitaji yao ya msingi kama Elimu sasa imefika wakati tunapaswa kutambua kuwa hilo ni tatizo kama matatizo mengine na tunachopaswa kukifanya ni kuwahudumia bila kuwanyanyapaa” alisema Urasa.

Aidha Urasa alisema kuwa, Wanawake wenye ulemavu, wamekuwa wakipata changamoto kubwa katika jamii, pindi wanapo olewa kwa kutotambua haki zao za msingi hivyo kituo cha Songambele kimekuwa kikiwaelimisha kujua haki zao pamoja na ujasiriamali ambapo wamekuwa wakitoa mitaji kwa mmoja mmoja.

Urasa alisema kuwa,  Familia ambazo wanatoka watu wenye ulemavu wamekuwa wakiwachukulia kama mzigo, na kuwatenga na jamii kwa kuwaficha ndani, hivyo ameiomba jamii kuungana kwa pamoja na kupaza sauti ili kuhakikisha kuwa walemavu hawatengwi.

Pia alisema kuwa, Serikali imekuwa na Sera ya watu wenye ulemavu, lakini jamii na baadhi ya viongozi wamekuwa hawaitekelezi, hivyo ameiomba Serikali kuhakikisha inaingilia ili  kuhakikisha kuwa walemavu wanapata haki sawa.

Awali Mkurugenzi wa kituo cha Gabriella, Brenda Shuma alisema kuwa, kutio chao kimekuwa kikiwahudumia watoto mbalimbali wenye mtindio wa ubongo kwa kuwapatia elimu ya darasani kwa vitendo pamoja na kuwafundisha masomo ya ujasiriamali, ambapo hufundisha kufuga kuku, mbuzi, sungura, mapishi na ushonaji.

Alisema kuwa, changamoto kubwa anayokumbana nayo, ni jamii kuwaficha watoto wenye mtindio wa ubongo, pamoja na kuwatenga kwa kuwanyanyapaa, bila kutambua kuwa nao wanahaki ya kupatiwa elimu.

Changamoto nyingine ni uhaba wa fedha kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao, pamoja na kuwalipa watumishi wanao wahudumia watoto hao kwani kituo hicho hakijafanikiwa kupata wafadhili.

No comments:

Post a Comment