Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, March 10, 2015

BREAKING NEWS: CHADEMA YAM'BWAGA ZITTO MAHAKAMANI                                Zitto Zubeir Kabwe

Mahakama kuu ya Tanzania, leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Zitto Zubeir Kabwe mwaka jana, akipinga kikao cha kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumjadili, akikitaka chombo hicho cha sheria, kukielekeza chama chake kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika baraza kuu.

Mahakama iliyoketi chini ya Jaji Mziray, ilikubaliana na hoja za mawakili wa CHADEMA, waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo ulikiuka baadhi ya vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Wakati Mheshimiwa Zitto
Zubeir Kabwe, akifungua kesi hiyo Januari mwaka 2013, tayari CHADEMA ilikuwa imewafukuza uanachama Dr. Kitilya Mkumbo na Samson Mwigamba ambao pamoja na Zitto Kabwe, walituhumiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi ya uongozi ndani ya chama hicho. Zitto Kabwe alikuwa akitetewa na wakili Albert Msando wakati CHADEMA iliwakilishwa na Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Mallya.

No comments:

Post a Comment