Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, March 10, 2015

Diwani wa kata ya Kia awahimiza wananchi kulipa michango kwaajili ya ujenzi wa maabara

KILIMANJARO wananchi kata ya Kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuwa wazalendo wa kulipa  mchango wa hela kwaajili ya ujenzi wa maabara  ili watoto wao waweze kuwa na fursa ya kupata elimu kama ilivyo kusudiwa.

Rai hiyo imetolewa jana na Diwani wa kata hiyo Sinyok Nairuk  alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa kata hiyo kwenye kikao cha (ODC) kilichofanyika  katika shule ya sekondari Kia, ambapo lengo kubwa lilikuwa ni michango wa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.

Nairuk alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiwapeleka shuleni watoto wao kwa lengo na kusoma lakini likija suale la kuchangia michango  mashuleni wamekuwa wakikaidi zoezi hilo jambo ambalo linarudisha elimu nyuma, hivyo amewaomba wazazi na walezi kwenye kata hiyo kuchangia michango hiyo.

Alisema kuwa mwisho wa kuchangia michango hiyo kwa hiyari ni tarehe 16 machi mwaka huu na baada ya hapo wataanza ubambuzi wa nyumba kwa nyumba hata kwa wafanyakazi wa uwanja wa kia ambao kwa kiwango kikubwa bado hawajatoa michango hiyo.

Kwa upande wake Afisa Tarafa masama Nsajigwa Ndagile aliwataka wananchi hao kumaliza michango hiyo mapema ili ujenzi huo uweze kumalizika kwa wakati kwani ni kwa faida ya watoto wao.

No comments:

Post a Comment