Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, March 3, 2015

KAMPUNI YA PANONE AND CO. LTD YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI

Mbio za Kilimanjaro Marathon ni Mashindano ya Riadha yanayofanyika kila Mwaka Mwishoni mwa mwezi wa Pili ndani ya Mji wa Moshi uliopo Mkoa wa Kilimanjaro. Mbio hizo ambazo hukutanisha mataifa Mbalimbali katika mji wa Moshi huku Makampuni Mbalimbali yakitumia Mbio hizo kuweza kujitangaza zaidi.
 MENEJA WA KAMPUNI YA PANONEAND CO. LTD NDUGU GIDO MARANDU AKIWA AMEPOZI NA AFISA MASOKO WA KAMPUNI HIYO NDUGU FRANK MWAIKATALE NJE YA BANDA LA PANONE KATIKA VIWANJA WA USHIRIKA.


WATEJA WAKITEMBELEA BANDA LA PANONE AND CO LTD NA KUNUNUA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA KAMPUNI HIYO 

Katika Mwaka huu Mashindano hayo yamefanyika siku ya jumapili ya tarehe 1/03/2015 kaika viwanja vya chuo kikuu cha Ushirika kilichopo Mjini Moshi. Jambo lililovutia zaidi ni kuhusu kampuni ya Panone and co. Ltd inayomiliki vituo vya Mafuta, Bekary na Hotel iliweza kuwakumbuka kundi maalumu la watoto ambao jamii imewasahau. Kampuni hiyo iliweza kujikita katika kuwapa nafasi watoto wenye ulemavu wa akili ambao wanaishi kaika kituo cha kuwalelea watoto hao kinachoitwa Gabriella.WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI WA KITUO CHA GABRIELA WAKIWA WAMEPOZI MBELE YA BANDA LAO BAADA YA KUMALIZA MBIO ZA KILOMETA 5 WALIZODHAMINIWA NA KAMPUNI YA PANONE AND CO. LTD.

Akiongea na Mtandao huu Afisa Masoko wa Kampuni ya Panone and Co. Ltd kwa kanda ya kaskazini ndugu Frank Mwaikatale alisema Kampuni ya Panone nd Co. Ltd imeona watoto hawa ni kundi ambalo jamii haiwapi nafasi na wameona ni vyema kuwapa nafasi katika mbio hizo ili waweze kujisikia nao wapo pamoja na jamii. Kampuni imeweza kuwalipia namba za kukimbilia watoto thelathini ambao ndio walikua na uwezo wa kukimia na kushiriki mbio za kilometa tano. Na pia imewea kuwapatia zawadi mbalimbali ambazo watoto hao walifurahia. 

 AFISA MSOKO WA KAMPUNI YA PANONE AND CO. LTD NDUGU FRANK MWAIKATALE AKIGAWA ZAWADI KWA WATOTO WA KITUO CHA GABRIELA WALIPOTEMBELEA BANDA LA PANONE.

Afisa masoko huyo alimalizia kwa kutoa wito kwa jamii pamoja na makampuni mengine kuweza kuiga mfano wa Panone and Co. ltd kaika kuisaidia jamii kutokana na Faida wanayopata mabayo inatoka katika jamii hiyo hiyo. Hata hivyo Mtandao huu uliweza kuzungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Gabriella kinacholelea watoto hao aliweza kutoa Shukrani a Dhati kwa kampuni ya Panone and Co. Ltd kwa kuweza kuwakumbuka watoto hao ambao wanauhitaji mkubwa wa Mahitaji pamoja na faraja kutoka kwa jamii huku akishukuru kwa niaba ya watoto kutokana na zawadi walizopata kutoka kampuni ya Panone and Co. Ltd.


MMOJA WA WAGENI WALIOJITOKEZA KUJIANDIKISHA KUKIMBIA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON AKIWA KATIKA POZI NA MABALOZI WA PANONE WALIOKUA WAKITOA VIPEPERUSHI VYA HUDUMA ZA KAMPUNI HIYO.


No comments:

Post a Comment