Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, March 5, 2015

Mkoa wa Kilimanjaro kujengwa uwanja wa nyasi utakaoingiza milioni 20 kwa mwezi

KILIMANJARO naibu waziri wa habari utamaduni na Michezo, Juma Nkamia ametoa miezi miwili kwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kuhakikisha wanaweka miundombinu mizuri katika uwanja wa Memorial, uliopo katika Manispaa hiyo.

Nkamia ametoa agizo hilo jana wakati alipotembelea na kujionea hali ya uwanja huo ambao uko katika hatua za awali za kujengwa na TFF.

Alisema endapo Manispaa hiyo watashindwa kuweka miundombinu hiyo ndani ya miezi ambayo ameitoa atawashauri TFF kuhamisha nyasi hizo na kupeleka katika viwanja vingine vyenye mahitaji kama hayo.

Aidha Naibu Waziri huyo, ametoa ushauri kwa Manispaa ya Moshi, kuzuia wafanyabiashara kutojenga majengo ya kudumu katika uwanja huo, na endapo watashindwa kutekeleza maagizo hayo yupo tayari kuwazuia TFF na
FIFA kuona maeneo mengine ambayo yanastahili kuwekewa nyasi bandia.

Kwa upande wake katibu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine,  alisema kuwa uwanja wa Memorial ni moja kati ya miradi ya viwanja ambavyo vimeombewa fedha kutoka kwa wafadhili ambao ni FIFA.

Selestine alifafanua kuwa FIFA inautaratibu wa kila mwaka kujenga uwanja wa nyasi bandia katika nchi nyingi zinazoendelea, ambapo tayari wamejenga uwanja wa Gombani Pemba, uwanja wa Uhuru, Karume, Nyamagana na Kaitabe.

Alifafanua kuwa katika mwaka huu, TFF imeombea fedha za kuujenga uwanja wa Memorial, lengo likiwa ni kila mkoa kuwa na uwanja wa nyasi bandia ambao utaliingizia taifa fedha nyingi.

“Kwa mkoa wa Kilimanjaro, ukiwa na uwanja wa nyasi bandia unauwezo wa kuingiza kiasi cha shilingi milioni 20 kwa mwezi, ambapo wafanyabiashara wataweza kunufaika na uwanja huu,” alisema
Selestine.

Awali akitoa taarifa kwa naibu waziri kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Erick Mapunda  alisema kuwa zaidi ya wafanyabiashara 200,000, wapo katika uwanja huo na wamekuwa pia wakiongeza pato la Manispaa kwa kiasi cha shilingi milioni 6 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment