Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, March 5, 2015

Wanasiasa pamoja na wananchi wametakiwa kuweka kando itikadi za kisiasa na kudumisha amani na upendo

KILIMANJARO viongozi mbalimbali wa siasa pamoja na wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanajaro wametakiwa kuweka kando itikadi za kisiasa na badala yake kujikita zaidi kujenga amani na upendo katika nchi hii ya Tanzania.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa ujenzi Jonh Mkufuli wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya kwasadala-masama ambayo inaendelea na kujengwa na mkandarasi mwingine baada ya yule wa awali kushindwa kukamilisha kazi, pia aliongea na wananchi wa kijiji cha Mula.

Makufuli alisema upendo na umoja kwa watu wote kutasaidia kuiweka wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla katika nafasi nzuri ya kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka zaidi.

Alisema wilaya hiyo ina nafasi kubwa ya kusonga mbele kimaendeleo hasa baada ya barabara hii kukamilika hivyo viongozi hao wana wajibu wa kuunganisha wananchi katika shughuli za kimaendeleo badala ya kuwafarakanisha kutokana na tofauti za kiitikadi za kisiasa alisema mkuu huyo.

Alifafanua suala la maendeleo kwa watanzania ni la kila mmoja bila kujali itikadi za siasa ndani ya nchi yenye mfumo wa vyama vingi.

Barabara hiyo yenye ukubwa wa km 12.5 inatarajiwa kukamilika  juni mwaka huu, kukamilika kwa barabara hii kutasaidia kukua kwa uchumi wa wilaya ya Hai.

No comments:

Post a Comment