Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, March 14, 2015

Mwalimu mstaafu atuhumiwa na jeshi la polisi kwa kuwahifadhi watoto wa kike 11 huko wilayani Hai

KILIMANJARO ikiwa bado wananchi mkoani Kilimanjaro wakiwa na hali ya sintofahamu, kuhusiana na tukio la kuhifadhi watoto 18, ndani ya nyumba moja kinyume na sheria za nchi.  Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limegundua tena  nyumba nyingine huko wilayani Hai  iliyokuwa ikiwahifadhi watoto 11 na kuwafundisha masomo ya dini ya kiislam na Ushonaji.

Jeshi hilo limegundua nyumba hiyo iliyopo katika kijiji cha Lyamungo wilayani Hai,  siku ya jumatano baada ya jeshi hilo kupokea taarifa  kutoka kwa wasamaria wema ambapo jeshi la polisi lilifika katika nyumba hiyo na kukuta watoto 11, wa kike wenye umri kuanzia miaka 14 hadi 17.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda Mwandamizi wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geoffrey Kamwela, alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa hizo, walifaka katika nyumba hiyo inayomilikiwa na Abubakari Juma(64), Mwalimu mstaafu wa shule za Msingi ambaye alifungua shule hiyo na kuipa jina la UMM SUKHAIL.

Kamwela alisema kuwa, watoto hao walikuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya Kiislam pamoja na Ushonaji ambapo walikuwa wakilala katika nyumba hiyo.
“Kweli tumegundua nyumba nyingine ambayo inafanya kazi ya kuwahifadhi watoto na kuwafundisha masomo ya dini pamoja na Ufundi cherehani kinyume na sheria ambapo mwenyenyumba na watoto hao wapo katika kituo cha polisi Moshi kati” alisema Kamwela.

Aliongeza kuwa katika uchunguzi wa awali na mahojiano ya watoto hao, inaonesha kuwa wanatoka katika mikoa ya Dodoma, Singida, Tanga, Tabora, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.

“Kama mtakuwa na kumbukumbu nzuri, katika tukio la kwanza la watoto 18, ukiangali mikoa waliyotoka na hili pia utagundua kuwa wote wametoka mikoa hiyo hiyo sasa nashindwa kuelewa kuwa hawa wamiliki wa nyumba hizi mbili wanafanya kazi pamoja au” alisema Kamwela.

Kamanda huyo aliwataja watoto hao kuwa ni Amina Yahaya(16),Mariam Issa(14), Zainabu Rajabu(16), wote wakazi wa Arusha, Idia Rashidi(15), mkazi wa Mbeya, Amina Adam(14), mkazi wa Tanga, Rehema Idd(16), mkazi wa Singida,Nasra Bashiri(16), mkazi wa Kilimanjaro.

Wengine ni Shahila Abdi(14), Salma Athumani(16), wote wakazi wa Dodoma, Hadija Ally(17), mkazi wa Mtwara, Amina Muhamedi(18).
Aliendelea kueleza kuwa, mmiliki wa nyumba hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro, kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kuwa shule hiyo aliyokuwa akiwafundishia watoto hao ipo kisheria na imesajiliwa pamoja na kutambua utoaji wa vyeti vya wanafunzi hao pindi wanapoitimu mafunzo.

Alisema kuwa endapo kutaonekana kuwa, mmiliki wa nyumba hiyo atakuwa amevunja sheria yoyote basi atafikishwa mahakamani na sheria kufuata mkondo wake.

No comments:

Post a Comment