Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, March 11, 2015

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania awaagiza maafisa michezo kuibua vipaji kwaajili ya baadae

KILIMANJARO Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Antony Mataka, amewaagiza Maafisa michezo mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanabaini vipaji mbalimbali vya michezo kwa vijana ili kuwa na wachezaji wazuri kwa
siku za baadae.

Mataka ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Hai, alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Novatus Makunga, ambaye amehamishiwa wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro huku Mataka akitokea
wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Mataka amewataka maafisa michezo hao kuacha kukaa ofisi, na badala yake watoke na kwenda vijijini ili kubaini vipaji vilivyoko katika maeneo hayo ili hapo baadae kuwa na wanamichezo wazuri ambao wataliwakilisha taifa katika medali za michezo.

Alisema malengo ya Shirikisho la Riadha hapa nchini ni kuhakikisha inazalisha ajira mpya kutoka kwenye makundi mbalimbali ya kimichezo ikiwemo mchezo wa Riadha, na kuwaomba wadau wa michezo kutoa ushirikiano kwa maafisa michezo hao kuweza kuwapata vijana wenye
vipaji vya michezo.

Aidha ameongeza kusema kuwa Tanzania imekuwa na wanariadha wazuri kutoka Kaskazini mwa Tanzania, hivyo endapo watatumiwa vema katika michezo sekta hiyo itazidi kukua ndani na nje ya nchi.

Wakati Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania Antony Mataka akitoa maelekezo kwa maafisa michezo, Serikali kupitia Wizara ya habari utamaduni na michezo iliiagiza shirikisho la Riadha la Tanzania (RT), kuweka mipango madhubuti kuzikabili changamoto ambazo imekuwa ikikabiliana nazo.

No comments:

Post a Comment