Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, March 18, 2015

Mwananchi ambaye hajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hataweza kupiga kura

SERIKALI, imesema mwananchi ambaye atakuwa hajajiandikisha kwenye daftari wa kudumu la wapiga kura  amepoteza fursa kwani kitambulisho kinachotumika  kwenye kura za maoni na uchaguzi mkuu ni kimoja. Kauli hiyo imetolewa  na Rais Jakaya, Kikwete wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya semina elekezi kwa wakuu wa wilaya wapya 27.

Rais alisema, endapo mtu atagoma kujiandikisha kwa maana amekatazwa na chama chake atakuwa amepoteza fursa kwani hakuna fursa nyingine tena. Aliwaagiza wakuu hao wa wilaya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuwaeleza umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lakini pia kujitokeza kwenye kura za maoni na kufanya maamuzi wanayoyataka.

Katika hilo aliwataka kutumia mamalaka yao ya ulinzi na usalama na  kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuamua wanachoona kinafaa kwa uhuru. Akizungumzia uchaguzi mkuu ameagiza uchaguzi huo kufanyika kwa amani na utulivu, wananchi wote wenye haki ya kupiga kura na wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaoona wanafaa.

Aliagiza kufanya maandalizi ya mapema kwa chaguzi zote na si kukurupuka wakati muda ikiwa umekwisha. Hata hivyo katika hotuba yake aliweza kuzungumzia suala la wahamiaji haramu, biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi  ambapo kwa hilo amezitaka kamati za ulinzi na usalama za wilaya kuhakikisha kuwa nchi inaondokana na mauaji hayo kwa kutengeneza mikakati maalumu ya kulipatia ufumbuzi suala hilo na kuwafanya watu wenye albinism waishi kwa amani kama binadamu wengine.

Kuhusu migogoro ya ardhi alisema kuwa matatizo ya migogoro ya ardhi ni lazima ishughulikiwe mara moja yanapotokea kwani yanapoachwa kwa muda ndipo yanapoleta shida na kufanya tatizo kuwa kubwa. Kwa upande wa ujangili wa wanyama pori Rais Kikwete alisema  kumekuwa na uvamizi mkubwa wa wanyamapori kama Faru, Simba, Chui ambapo wengine wanatafutwa kutokana na ngozi zao na wengine kutokana na pembe zao.

No comments:

Post a Comment