Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, March 18, 2015

Mwenyekiti akemea vitendo vya wanafunzi na vijana kucheza kamari, pool table na kushinda kwenye vibanda umiza

KILIMANJARO mwenyekiti wa Kijiji cha Sanya Hoyee Mtaa wa Mabanzini Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro, Moses Munuo, kupiga marufuku vibanda vya video kuonesha picha nyakati za asubuhi pamoja na kucheza "pool teble" kwa kile anachodai kuwa vijana na wanafunzi wanashindwa kutimiza wajibu wao kwa kuishia kwenye vibanda hivyo.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti huyo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari Ofisini Kwake, alisema kuwa watoto wao wanashindwa kuhudhuria masomo darasani na badala yake wanaishia kwenye vibanda vya video wanacheza kamari kwenye vilabu vya pombe na wengine kucheza mchezo wa "pool table" jambo ambalo ni hatari kama litanyamaziwa.

Alisema  katika harakati za kuokoa uchumi wa Taifa hili masikini, Vijana wa kiume ambao wana nguvu za kufanya kazi za uzalishaji mali ni marufuku kucheza kamari maeneo ya
vilabu vya pombe hasa hizi kamari za kichina, "pool teble" pia kuonesha picha nyakati za asubuhi, pia nyakati za usiku watoto wadogo wasiruhusiwe kuingia kwenye vibanda hivyo

Wilaya yetu inamaeneo makubwa ya kufanya kazi hasa za kilimo na ukizingatia msimu huu ni wa kilimo unashangaa kuona vijana wakiangalia picha asubuhi na wengine wakicheza michezo isiyokuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla


Kuanzia sasa ni marufuku kwa vibanda hivyo kuonesha picha nyakati za asubuhi, kucheza kamari na atakae kiuka taratibu hizi sheria itachukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment