Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, March 18, 2015

Rais awaasa wakuu wa wilaya kutojiingiza kwenye ulevi kupindukia, madeni kupindukia na matumizi mabaya ya madaraka

DODOMA Rais wa jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete, amekemea vitendo vinavyotia aibu uteuzi wake, vya ulevi kupindukia, madeni ya kupindukia na matumizi mabaya ya madaraka vinavyofanya na wakuu wa Wilaya nchini.Aidha, ni moja ya sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa baadhi ya wakuu wa wilaya aliokuwa amewateua.

Kikwete ametoa, kauli hiyo mjini dodoma  wakati alipokuwa akifungua semina elekezi ya wakuu wa wilaya wapya 27, ya siku 4 inayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya mtakatifu Gaspari. Alisema wakati mwingine anapopokea taarifa za mambo machafu yanayofanywa na wakuu wa wilaya katika maeneo yao amekuwa akitamani yasiwe ya kweli.

Amesema yeye kama rais wa nchi ana mamlaka makubwa sana lakini hatumii madaraka yake vibaya iwaje wao wawe wanatoa amri za kuwaweka watu ndani bila sababu za msingi.

Rais amesema, serikali ina majukumu matatu ambayo ni utawala, usalama na maendeleo amabayo huko wilayani yanasimamiwa na mkuu wa wilaya ambaye ndiye muwakilishi wa rais, anatakiwa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa sawa.

Akizungumzia ujenzi wa maabara ambapo ameongeza muda mpaka Juni mwaka 2015, aliwataka wakuu hao kutokuwa na kisingizio chochote kwamba ni wateuzi wapya bali wahakikishe muda unapofika maabara ziwe zimekamilika katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment