Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, March 6, 2015

Serikali imeahidi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayojitokeza ili kuepusha majanga

KILIMANJARO serikali imeahidi  kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayojitokeza mara kwa mara ili kuepusha majanga yanayojitokeza hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Siha, Dkt Charles Mlingwa, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Matokeo ya utekelezaji wa Mradi wa kupunguza uharibifu wa Ardhi katika sehemu za miinuko ya mlima Kilimanjaro,  mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uhuru hotel mjini Moshi.

Alisema  mradi wa matumizi endelevu ya ardhi (SLM), umeweza kuwa na mafanikio makubwa kutokana na  juhudi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kwa kushirikisha sekta binafsi na mashirika yasiokuwa ya kiserikali.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa matumizi endelevu ya ardhi mkoa wa Kilimanjaro, Damas Masologo alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa mkoa umefanikiwa kwa asilimia 70.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi, Msimamizi wa mradi kutoka (UNDP), Getrud Lyatuu alisema miradi hiyo ilikuwa ni miradi ya majaribio, katika sekta ya Kilimo, utunzaji wa mazingira uzalishaji mali, na ufugaji.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Siha, Rashid Kitambulilo, alisema miradi ya SLM, imekuwa na mafanikio makubwa, na kwamba halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 150 ili kuendeleza utekelezaji wa miradi katika ambyao hayafikiwa na mradi.

Mkutano huo wa kanda umezishirikisha nchi za Uganda , Malawi, Kenya na wenyeji Tanzania.

No comments:

Post a Comment