Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, March 10, 2015

Tundu Lissu atangaza rasmi kuwa Zitto Kabwe si mwanachama wa CHADEMA





Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.



kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe. "Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema"


Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.

Chanzo: eatv.tv.news


No comments:

Post a Comment