Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, April 7, 2015

Jumla ya watoto 53 wazaliwa katika juma la sikukuu ya PasakaDODOMA jumla ya Watoto 53 wamezaliwa kwenye Juma la Sikukuu ya Pasaka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Dodoma.
Kati ya Watoto hao waliozaliwa wa kike ni 23 na wa kiume 30.

Akizungumza na waandishi wa habari Muuguzi wa zamu katika Hospitali hiyo ya Rufaa, Dina Msesa alisema kati ya watoto hao waliozaliwa kwa njia ya upasuaji ni watoto 10, kwa njia ya kawaida watoto 43 na waliozaliwa wakiwa wamefariki ni wawili.


Aidha alisema kuwa katika Juma hili la Sikukuu ya Pasaka kati ya watoto hao wamezaliwa 53 mtoto mmoja alizaliwa kwa njia ya kuvutwa na yupo salama yeye pamoja na Mama yake. Hata hivyo alisema wanakabiliwa na Changamoto ya kukosa sehemu ya kuwalaza kina Mama wajawazito hali ambayo hupelekea kuhamishwa na kupelekwa katika kituo cha afya cha Makole kilichopo mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment