Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 23, 2015

Idadi ya wagonjwa wa Minyooo na Kichocho mkoani Kilimanjaro mwaka 2014 ni 57,014


SERIKALI mkoani Kilimanjaro imesema magonjwa ya Minyooo na Kichocho yanaongoza kwa kuaathiri afya za wananchi wengi mkoani hapa ambapo mwaka jana(2014) jumla ya wagonjwa 57,014 waliofika katika vituo vya afya waligundulika kuugua magonjwa hayo na kupatiwa matibabu.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ameyasema hayo wakati akifungua warsha ya uhamasishaji juu ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTD) kwa Wakurugenzi na Wenyeviti wa halmashauri, wataalamu wa afya na elimu wa wilaya kutoka mkoani Kilimanjaro.

Akifungua warsha hiyo ya siku moja Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Alfred Shayo, amesema Magonjwa ya Minyoo na Kichocho yanaongoza kwa kuathiri afya za wakazi wengi wa mkoa wa Kilimanjaro kutokana na kupuuzia kuchukua taadhari mapema ambapo wilaya ya Hai inaongoza kwa wagonjwa 12,012 wa minyooo.

Amesema wilaya ya Rombo inakamata nafasi ya pili ya wagonjwa 10,753 walitambulika wilayani humo na kwamba katika kipindi hicho wagonjwa 1,445 waligundulika kuwa na ugonjwa wa kichocho na wilaya ya Same iliongoza kwa kuwa na wagonjwa 529 ikifuatiwa na Manispaa ya Moshi iliyokuwa na wagonjwa 359 wagonjwa waliofika katika vituo vya afya.

Mhandisi Shayo amesema magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni magonjwa ambayo yanaathiri jamii ya watu wenye kipato cha chini wanaoishi katika maeneo duni maeneo ambayo upatikanaji wa huduma za afya na maji safi na salama ni mgumu.

Mhandisi Shayo ametaja magonjwa mengine kuwa ni pamoja na ugonjwa wa Matende na mabusha, Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo ya tumbo, Homa ya malale, kichaa cha Mbwa, Tauni na Tegu na kwamba athari za magonjwa hayo yasipotibiwa mapema ni pamoja na Saratani ya kibofu cha mkojo na ini, upofu, Utumbo kujifunga na dalili za kifafa.

Amefafanua kuwa maambukizi ya magonjwa hayo yanatokana na kuenezwa na wadudu kama Inzi, Mbu na Konokono, na magonjwa hayo husababisha pia ulemavu wa kudumu hali ambayo inawapunguzia wananchi uwezo wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi.

Shayo ametoa wito kwa viongozi kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi wote kuzingatia usafi wa mazingira na kumeza dawa za kingatiba kwani wakazi wengi wa mkoa wa Kilimanjaro hususani jamii ya watu wenye kipato cha chini.

No comments:

Post a Comment