Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 16, 2015

Wajumbe wa Imetosha wawasili Mwanza kwa ziara ya siku tatu

Katibu wa Imetosha Salome Gregory akifuatiwa na Balozi Mdimu na Issaya Mwakilasa(wakuvawga) wakiteremka toka ndegeni leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Toka kushoto Wakuvwanga, Zaytuni Biboze, Salome Gregory, Henry Mdimu na  msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika wakiwa nje ya uwanja wa ndege jijini Mwanza mara baada ya kuwasili leo asubuhi

 

Wajumbe wa taasisi ya Imetosha inayojishughulisha na utoaji elimu juu ya kumaliza unyanyapaa,  ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini uliwasili jijini Mwanza leo hii saa 2 asubuhi kwa ziara ya siku 3 ambapo kati siku hizo tatu ujumbe huo utakutana na viongozi wa ki serikali na usalama wa baadhi ya mikoa na wilaya za kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Shinyanga. Lengo la mikutano hiyo ni kamati kujitambulisha kwa viongozi hao na kuwaeleza nini Imetosha inatarajia kufanya katika kanda hii mwezi ujao ambako pamekuwa na matukio mengi ya ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania. 

Vile vile kamati itakuwa na siku moja ambapo itatembelea vyombo ya habari vya jijini hapa kabla ya kurejea Dar es Salaam.

Habari na picha na Mkala Fundikira wa Mkalamatukio/keronyingi blog

No comments:

Post a Comment