Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 16, 2015

Wakazi wa vijiji 39 watishia kususia zoezi la kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2015KILIMANJARO wakazi
 wa vijiji thelathini na tisa (39) wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), wametishia kususia zoezi la kupiga kura ya kuwachagua Wabunge, Madiwani na Rais katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu kutokana na kuzuiliwa na serikali kutumia eneo nusu maili walilopanda miti ili kujipatika malisho ya mifugo na kuni.


Wakazi hao waliyasema hayo jana wakati wakimsindikiza Askofu Mkuu Mstaafu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Dk,Martin Shao, wakati alipokuwa akikabidhiwa mizinga ya nyuki na Shirika lisilo la kiserikali linalijihusisha na uhifadhi wa mazingira Mkoani Kilimanjaro TEACA.

Wananchi hao wamesema wanakusudia kutoshiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na na serikali kupitia Kinapa kuwazuia kutumia eneo hilo kwa ajili ya kupanda miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na wao kujipatia kuni na malisho ya mifugo.

Walisema wamekuwa wakilitunza eneo hilo kwa kupanda miti, kila mwaka na kwamba wanashangazwa na uongozi wa KINAPA, kuwazuia kupanda miti katika eneo hilo ambalo lipo wazi baada ya miti iliyokuwapo huko nyuma kuvunwa na kuachwa jangwa.

Mwenyekiti wa hifadhi ya mazingira wa Kata ya Mwika Kaskazini, Nderingo Mringo, alisema kuwa viongozi wamekuwa wakifika katika eneo hilo na kutoa ahadi za uongo kuwa eneo hilo litarudishwa kwa wananchi ili waweze kujipatia mahitaji yao madogo madogo huku wakiendelea kulitunza eneo hilo ahadi ambazo zimekuwa hazitekelezeki hadi sasa.

Aidha Mringo alifafanua kuwa wananchi wa kijiji hicho ambacho ni moja ya vijiji vinavyozunguka hifahdi hiyo, wamekuwa wakibakwa na baadhi ya askari wa Kinapa pindi wanapoingia katika hifadhi hiyo kwa lengo la kukata majani ya ng’ombe na kuni kwa ajili ya matumizi ya majumbani.

Awali akikabidhi mizinga hiyo ya nyuki, kwa Askofu Martine Shao, Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali TEACA linalojishughulisha na shughuli za utunzaji na uhifadhi wa mazingira wilaya ya Moshi vijijini mkoani hapa Ozeniel Foya, aliwataka wananchi hao kufuga nyuki ili waweze kujiongezea kipato na kuwainua kiuchumi na hivyo kuondokana na umasikini kwa kuwa ufugaji huo ni moja ya shughuli za maendeleo.

Foya amewashauri wananchi kuondokana na dhana ya kutegemea msitu pekee wa nusu Maili kwani fursa hiyo waliyoipata ni nzuri na hivyo ni vyema wakaitumia kwa ufugaji wa nyuki ambapo mazao yake yanafaida kubwa kwani asali inafaida kubwa ili waweze kujiingizia kipato kuliko kutegemea mazao ya Msitu.

Kwa upande wake Askofu Mkuu Mstaafu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Dk,Martin Shao, amelipongeza shirika la TEACA kwa msaada huo wa mizinga ya nyuki, ambayo itamwezesha kuzalisha asali na kujiongezea kipato.

No comments:

Post a Comment