Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, April 17, 2015

Mahakama wilaya ya Hai imeondoa shauri la wizi wa kiasi cha shilingi 10,611,450 za kitanzania


KILIMANJARO mahakama ya wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imeondoa shauri la wizi wa fedha ya kitanzania 10,611,450 mali ya SACCOS ya wazazi Siha lililokuwa likimkabili aliyekuwa katibu wa jumuiya ya wazazi wa CCM Wilaya ya Siha Ally Ballo(49)

Kuondolewa kwa shauri hilo la jinai namba 333 ya 2014 kunatokana na maombi yaliyotolewa na shaidi namba moja wa kesi hiyo Herman Mlale ambaye pia ni Mwenyekiti wa SACCOS kutokana na kutoridhishwa na upelelezi wa awali uliofanywa na Jeshi la polisi kituo cha Sanya Juu.

Akitoa ombi hilo mahakamani hapo mbele ya Hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo, Agnesi Mhina, Mlale amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haukuzingatia vigezo vyote hali inayosababisha kutoa ombi hilo ili waweze kufanya utaratibu wa kumpata mwanasheria binafsi aweze kufanya upelelezi kwa upya na kuendesha shauri hilo. 

Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Siha, Roymax Membe alisema kuwa upande wa mashitaka na mahakama hauna pingamizi juu ya ombi hilo na kumtahadharisha mlalamikaji mambo mbalimbali ya kisheria ili kukidhi haja hiyo ikiwemo mazingira finyu ya uwezekano wa ombi hilo. 

Membe alisema ameridhika na ombi na kuishawishi mahakama kukubali ombi la mlalamikaji kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 98 (a) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 ya mwaka 1985 na mahakana kumwachia huru Mtuhumiwa Ally Ballo ili kuruhusu mlalamikaji kuendelea na utaratibu anaoutaka. 

Hata hivyo mnamo Machi 25 mwaka huu mlalamikaji wa shauri hilo Mlale alitoa ombi la kuhairishwa kwa kesi hiyo ili kuweza kutafuta msuluhishi ya nje ya makahama jambo ambalo alidai kuwa lilishindikana kutokana na kukosa mpatanishi.

No comments:

Post a Comment